Tuesday, March 22, 2016

MWANAFUNZI ALAZWA HOSPITALI BAADA YA KUUMWA NA NYOKA



Na Steven Augustino,
Tunduru.

MWANAFUNZI anayesoma darasa la saba shule ya msingi Msamaria, iliyopo kijiji cha Mtangashari wilayanai Tunduru mkoa wa Ruvuma, Ramadhan Swedi (14) amelazwa katika Hospitali ya wilaya hiyo, baada ya kuumwa na nyoka.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa, mwanafunzi huyo alikumbwa na mkasa huo wakati akiwa anacheza mpira na wenzake katika maeneo ya shule hiyo.

 Mzazi wa mwanafunzi huyo, Usale Swedi alisema baada ya tukio hilo kutokea walimu walimpatia huduma ya kwanza ya kumfunga kamba na kumnywesha mafuta ya taa, na baadaye kumpeleka nyumbani kwake.


Alisema, baada ya tukio hilo wanafamilia walilazimika kubeba jukumu la kumpeleka hospitali, kwa matibabu   zaidi ili kuokoa maisha yake.

Swedi aliwapongeza waganga na wahudumu wa hospitali hiyo, kwa jitihada walizozifanya utoaji wa huduma kwa mtoto huyo, ingawa bado wamelazwa kwa ajili ya matibabu lakini hali yake inaendelea kuimarika.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Tunduru, Dkt. Mmari Zabron alikiri kumpokea majeruhi huyo, Marchi 15 waka huu. 

Alisema hivi sasa hali yake inaendelea vizuri na maofisa tabibu, wanaendelea kumpatia matibabu ili kuokoa maisha yake.

No comments: