Friday, June 16, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: MIUNDOMBINU CHAKAVU YA MAJENGO SHULE YA MSINGI MALOMBE TUNDURU MKOANI RUVUMA

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Brawn Mwangomale (Katikati) aliyenyoosha mkono akipokea maelekezo kutoka kwa walimu wa shule ya msingi Malombe iliyopo katika kata ya Mlingoti wilayani humo, wakati alipotembelea katika shule hiyo kwa lengo la kujionea miundombinu ya madarasa ya shule hiyo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama hicho katika ngazi ya kijiji na kata hiyo, wakati walipotembelea miongoni mwa nyumba ambazo wanaishi walimu hao wanaofundisha katika shule ya msingi Malombe wilayani Tunduru.
Baadhi ya walimu wa shule ya msingi Malombe wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya nyumba anayoishi mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Malombe. (Picha zote na Steven Augustino)

No comments: