Monday, June 12, 2017

RAIS DOKTA MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA PILI KAMATI YA UCHUNGUZI WA MADINI HAPA NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga, unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi, kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumkabidhi Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hiyo ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Madini Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi, Mwenyekiti wa kamati ya pili ya Madini Propfesa Nehemiah Osoro pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo waliojumuika na viongozi wa Dini Ikululeo Jjijini Dar es Salaam. 

Wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia kwa makini Ripoti hiyo ya pili ya Kamati ya Madinileo Ikulu Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Ikulu)

No comments: