Thursday, June 22, 2017

RAIS DOKTA MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA BAGAMOYO MSATA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mama Salma Kikwete (Mbunge), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa barabara ya Bagamoyo - Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la daraja la Ruvu chini Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete, Katibu wa itikadi na uenezi CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa serikali na Wabunge, akivuta kitambaa kuashiria jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bagamoyo - Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bagamoyo - Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya barabara hiyo ya Bagamoyo - Makofia Msata kama inavyoonekana katika picha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kufungua barabara ya Bagamoyo - Makofia Msata katika eneo la daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.(Picha zote na Ikulu)

No comments: