Tuesday, June 13, 2017

SPIKA AWAONYA WAPINZANI WANAOTAKA MARAIS WASTAAFU WASHTAKIWE

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewakumbusha Wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, akiwaeleza kuwa wanapaswa wakumbuke pia wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao nao watahusika pia.
Job Ndugai.

Ndugai alisema hayo leo Bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali akisema kuwa haiwezekani Mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.

Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu, Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe”, alisema Lijualikali.


Baada ya Mbunge huyo kutoa hoja hiyo ambayo inafanana na ya Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche, Spika wa Bunge Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.


Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena”, alisema Ndugai.

No comments: