Sunday, June 18, 2017

WAZIRI MKUU AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA KANISA KATOLIKI ZUZU DODOMA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa upande wa kushoto akiwa ameongozana na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu Pinda walipokuwa wakimpokea katika makazi yao yaliyopo Zuzu nje kidogo mjini Dodoma June 17 mwaka huu wakati wa kuhudhuria Misa ya kumbukumbu ya marehemu mzee Exavery Pinda, Baba mzazi wa Mizengo Pinda, pamoja na kuongoza uchangiaji wa ujenzi wa nyumba ya Paroko na ukarabati wa Kanisa la Parokia ya Zuzu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya familia yake akimkabidhi mchango wa shilingi milioni kumi, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia ukarabati wa Kanisa Parokia ya Zuzu Dodoma. Upande wa kushoto ni msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga. Harambee hiyo ilifanyika June 17 mwaka huu katika makazi ya Waziri Mkuu mstaafu Pinda, yaliyopo Zuzu nje kidogo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda akiwaonyesha Wageni waalikwa ambao hawapo pichani shilingi milioni 10 ambao ni mchango aliokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kwa niaba ya familia yake kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya Paroko pamoja na kufanyia ukarabati wa Kanisa Parokia ya Zinje (Zuzu) Dodoma. Kushoto ni msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: