Sunday, June 18, 2017

WATOTO WALIONUSURIKA AJALI YA LUCKY VINCENT KUREJEA HAPA NCHINI BAADA YA MIEZI MIWILI

WATOTO watatu ambao walinusurika katika ajali iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na Dereva wa shule ya Lucky Vincent mjini Arusha, huenda wakaruhusiwa kurejea hapa nchini baada ya miezi miwili.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ametoa taarifa hiyo katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii yaani Facebook.

Nyalandu katika ukurasa huo ameandika akiwataja watoto hao kuwa ni Doreen Mshanga, Saidia Ismael na Wilson Tarimo wanategemewa kutembea tena.

Kadhalika hivi sasa Doreen, atahamishiwa katika kituo maalumu cha Madonna kwa ajili ya matibabu ya uti wa mgongo kilichopo mji wa Lincoln, Nebraska.

“Katika watoto wote hao watatu, Doreen ni muujiza mkubwa zaidi,” alisema Nyalandu.

No comments: