Wednesday, June 28, 2017

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WATAALAMU WA NISHATI KUTOKA ETHIOPIA NA TANZANIA PAMOJA NA KAMATI YA UCHUNGUZI MCHANGA WA MADINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa maji, umwagiliaji na umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele anayeongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo hapa nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Steigler’s Gorge leo Ikulu Jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa maji, umwagiliaji na umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Steigler’s Gorge leo  Ikulu Jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati mbili alizoziteua za uchunguzi wa mchanga wa Madini (Makinikia) leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa maji, umwagiliaji na umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Waziri wa maji, umwagiliaji na umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele baada ya kupata picha ya pamoja na ujumbe wake kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa bwawa hilo wakiwa pamoja na jopo la wataalamu wa Tanzania wanaosimamia mradi huo leo Ikulu Jijini Dar es salaam. (Picha zote na Ikulu)


No comments: