Wednesday, September 6, 2017

KAMATI TEULE YA BUNGE YABOMOA VIGOGO WA SERIKALI

Na Mwandishi wetu,

KAMATI teule ya Bunge zilizopewa dhamana ya kuchunguza madini ya Almasi na Tanzanite zimewasilisha ripoti hiyo kwa Spika wa bunge, Job Ndugai huku baadhi ya vigogo wakiwa wamekalia kuti kavu.

Ripoti hizo mbili zilizowasilishwa leo ziliwataja vigogo hao wakiwemo, mawaziri wa sasa, mawaziri wa zamani pamoja na mwanasheria wa serikali.

Wenyeviti wa kamati hizo waliwataja baadhi ya vigogo akiwemo aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, aliyekuwa mwanasheria wa serikali Fredrick Werema, Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene, Profesa Sospeter Mhongo, Edwin Ngonyani pamoja na watendaji mbalimbali wa serikali.


Kwa nyakati tofauti kamati hizo zilisema kuwa kamati hizo zimebaini kuwepo kwa madudu mbalimbali huku viongozi katika nyadhifa mbalimbali kwa uchimbaji wa madini ya Tanzanite pamoja na Almasi mbalimbali wakionyesha.

Vilevile kamati hizo za uchunguzi wa madini ya Almasi na Tanzanite zimekuwa mwiba mkali kwa baadhi ya vigogo wa serikali pamoja na baadhi ya viongozi wakubwa ambao ni wastaafu.

Katika kamati ya Almasi iliyowasilishwa na Mussa Azan Zungu hivyo taarifa ya Almasi, imesikitishwa na kampuni ya uchimbaji wa almasi kumzawadia kiongozi mkubwa ambaye alikuwa serikalini almasi yenye thamani ya dola milioni 20.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mussa Azan Zungu alisema wamebaini kuwepo kwa madudu mengi katika uchimbaji wa madini ya Almasi.

Alisema kuwa licha ya kuwa kuna madudu mengi, lakini bado maeneo mengi ya uchimbwaji wa madini ya Almasi hayajafanyiwa utafiti wowote.

Zungu alifafanua kuwa utaratibu wa uchimbaji wa Almasi unafanywa kiholela huku akisema kuwa bado kampuni nyingi zimekuwa vinara wa kukwepa kulipa kodi au kubadilishana majina ya makampuni kwa madai ya kusingizia kupata hasara.

Akizungumzia kampuni ya uchimbaji wa madini ya Williamson, tangu mwaka 2007 hadi 2017 haijawahi kulipa kodi.

Alisema kuwa kampuni hiyo haikuweza kulipa kodi na Mrabaha kwa kisingizio kwamba inapata hasara, huku akihoji kama kweli kampuni inapata hasara kwa nini isifunge virago.

Vilevile kamati imebaini kuwepo kwa taarifa tofauti kwamba taasisi za serikali ambazo zinahusika katika sekta ya madini.

Hata hivyo kamati ilisema kwamba madini mengi ya Almasi yamekuwa yakiuzwa bila kulipia kodi hatua ambayo imeipotezea fedha nyingi serikali ambazo zingetumika kuleta maendeleo ya wananchi.


No comments: