Thursday, September 7, 2017

WANASHERIA KENYA WALAANI VIKALI TUKIO LA KUPIGWA RISASI TUNDU LISSU

Kenya. CHAMA cha Wanasheria nchini Kenya (LSK) kimelaani vikali tukio la kupigwa risasi Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu.

Rais wa LSK, Isaac Okero amesema tukio hilo limewashtua wanasheria wote wa Kenya.

“Tumepata taarifa kwamba Lissu amepigwa risasi akiwa kwenye gari lake mjini Dodoma, kwa kweli imetushtua sana na inahuzunisha,” amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.


“Kwa pamoja tunalaani tukio hilo kwa kuwa hili limewagusa wanasheria wote wa Afrika na hata dunia kwa jumla. Tunasikitika kwa uvunjifu wa sheria uliofanyika,’’ amesema.

Amesema kuwa Lissu anafahamika kwa kutetea haki za binadamu, hivyo wanasheria wote wapo pamoja naye katika kipindi hiki kigumu kwake na Mungu atamsaidia atarudi katika hali yake ya kawaida.

Mwananchi:


No comments: