Monday, September 4, 2017

WATAALAMU WATEGUA BOMU LA VITA KUU YA DUNIA

WATAALAMU wa kutegua mabomu mjini Frankfurt, Ujerumani siku ya Jumapili walifanikiwa kutegua bomu kubwa ambalo halikuwa limelipuka kwa miaka mingi na lilikuwa limeunganishwa wakati wa Vita kuu ya pili ya dunia.

Bomu hilo ambalo ni la tani 1.4 kutoka Uingereza liligunduliwa katika eneo la ujenzi siku ya Jumatano.

Habari hizo zilipokelewa kwa shangwe na watu zaidi ya 65,000 ambao walikuwa wamehamishwa maeneo yao kwa sababu za kiusalama baada ya bomu hilo kuteguliwa.


Hiyo ilikuwa idadi kubwa zaidi ya watu kuhamishwa tangu kutokea kwa Vita hivyo nchini Ujerumani na shughuli hiyo ilihusisha mamia ya maafisa wa serikali.

Maeneo ambayo watu walihamishwa yalikuwa katika mtaa wa Westend pamoja na hospitali kadhaa, nyumba za kuwatunza wagonjwa na hata katika Benki kuu ya Ujerumani.


Inaaminika kwamba kuna mamia ya maelfu ya mabomu ya wakati wa vita kuu ya pili ya dunia ambayo hayakulipuliwa ambayo yametapakaa kote Ujerumani.

No comments: