Monday, September 4, 2017

SOKABETI YALAMBISHA DILI LA MAMILIONI YA FEDHA TIMU YA MAJIMAJI SONGEA

Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji Songea, Steven Ngonyani upande wa kulia na Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda wakisaini mkataba wa kuidhamini timu  hiyo.
Na Mwandishi wetu,

KAMPUNI ya Mchezo wa Kubashiri ya Sokabet, imezinduliwa rasmi leo Jumatatu, Septemba 4 mwaka huu katika Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam.

Katika hafla ya uzinduzi huo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanasoka wa zamani pamoja na waandishi wa habari huku ikishuhudiwa kampuni hiyo ikiingia mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Majimaji ya Songea, wenye thamani ya shilingi milioni 150.

Mratibu wa Sokabet, Franko Ruhinda alisema kuwa wanayo furaha kuona leo hii wanazindua rasmi Sokabet ambayo itawapa fursa wadau wa kubeti kujishindia mamilioni kwa dau dogo tu watakaloweka kwenye kubashiri kwao michezo mbalimbali ikiwemo soka na ngumi.


“Lakini pia tunayo furaha zaidi kuingia mkataba na Majimaji ambapo kupitia timu hii inayoshiriki Ligi kuu bara, Sokabet itatangazwa kila kona na kujulikana zaidi nchi nzima”, alisema.

Kadhalika, Franko aliongeza kuwa kampuni hiyo ya Kitanzania inaanza ikiwa na mikakati mingi ya kusaidia jamii kwa kile ambacho kitakuwa kikipatikana kutokana na kubashiri, ambapo washiriki wanaweza kujiunga kwa kuingia katika tovuti ya www.sokabet.co.tz.

Naye Mwenyekiti wa Majimaji, Steven Ngonyani alisema kuwa wanashukuru udhamini huo wa Sokabet kwani utaweza kuwaongezea kitu kwenye timu hiyo hususani katika kujiendesha msimu mzima wa ligi hiyo ambao una mambo mengi lakini pia wataitangaza kampuni popote waendapo.


No comments: