Friday, March 9, 2018

HALMASHAURI MADABA KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU MBALIMBALI

Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma, Pololet Mgema akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha pili, Cosma Mwageni (Katikati) na Happy Hyera wa shule ya Sekondari Mahanje Halmashauri ya Wilaya Madaba Mkoani humo, wakati alipotembelea kukagua ujenzi ambao unaendelea wa mradi wa mabweni, vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo ambapo upande wa kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Shafi Mpenda.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma, Shafi Mpenda aliyevaa suti akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani humo, Pololet Mgema baadhi ya vitanda vilivyowekwa katika moja ya bweni ambalo limejengwa na Serikali kupitia mpango wa P 4 R katika shule ya Sekondari Mahanje iliyopo Wilayani hapa.


Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma, Pololet Mgema upande wa kulia akikagua ujenzi wa chumba cha Wodi ya akina mama na watoto inayojengwa katika Kituo cha afya Madaba, ikiwa ni lengo la kuboresha huduma za tiba kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoani humo.


No comments: