Saturday, March 10, 2018

MWENYEKITI AOMBA MSAADA DAKTARI WA KUITIBU MAJIMAJI SONGEA



Na Kassian Nyandindi,     
Songea.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Ruvuma, Golden Sanga amesema kuwa hali ya maendeleo ya timu ya soka ya Majimaji Mkoani humo, hivi sasa imeyumba na kwamba hawana uhakika wa kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi. 

Aidha Sanga amefafanua kuwa hawako vizuri kifedha, jambo ambalo linasababisha kukosekana kwa matokeo mazuri ndani ya timu yao, ambayo ipo mwisho wa msimamo wa ligi ya VPL.

Alieleza kuwa timu haijasimama vizuri kutokana na baadhi ya wachezaji kusimamishwa, ambao hawajatajwa na sababu za kusimamishwa kwao hazijawekwa wazi.


Kadhalika Mwenyekiti huyo ameweka wazi suala la kutokuwa na maelewano kwa baina ya viongozi Klabuni, suala ambalo amedai kwamba linakuwa pia sababu ya kuendelea kukalia mkia katika msimamo wa ligi hiyo.

Uwepo wa changamoto hizo, umemlazimu Sanga kusema wanahitaji madaktari ili aweze kuwasaidia kuyatibu matatizo waliyonayo kwa maana yamekuwa sugu sasa.

Hata hivyo Majimaji itaingia Uwanjani 'Sabasaba Stadium' ikiwa na alama 15 tu, kucheza dhidi ya Lipuli FC kutoka Iringa.

No comments: