Monday, March 5, 2018

MSAFARA WA POLEPOLE WAPATA AJALI KASULU



Na Mwandishi Wetu,

MSAFARA wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Hamphrey Polepole umepata ajali katika eneo la kijiji cha Nyamidaho, Kata ya Makere Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota V8 yenye namba za usajili T 150 EWE iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la, Kibuta wakati wakielekea leo katika ziara ya kiongozi huyo Wilayani Kakonko, Mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma, upande wa kulia.


Kwa mujibu wa Kamanda Otieno alisema kuwa waliojeruhiwa ni pamoja na Katibu wa CCM Mkoa, Naomi Kapambala, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sylivia Sigura pamoja na Katibu Mwenezi, Feruz ambao wamekimbizwa katika Hosiptali ya Wilaya ya Kibondo kwa matibabu zaidi.

Polepole amewasili leo Mkoani Kigoma na kupokelewa Wilayani Uvinza akitokea Mkoa wa Tabora ambapo atakuwa Kigoma kwa takribani siku tatu katika ziara yake kikazi.

No comments: