Saturday, March 10, 2018

WANAOANZISHA CHOKOCHOKO WAMCHUKIZA DOKTA MAGUFULI



Na Mwandishi wetu,

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli amewapongeza Wizara ya Ujenzi na Mkandarasi aliyefanikisha ujenzi wa barabara ya Uyovu – Bwanga na kudai kuwa watu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sio ndiyo wanawahi kwenda kuandamana.

Dokta Magufuli alisema hayo leo Machi 10 mwaka huu akiwa kwenye ufunguzi wa barabara hiyo, Bukombe Mkoani Geita na kusema kuwa Serikali imefanya maendeleo makubwa ujenzi wa barabara hapa nchini na kudai hayo ndiyo mambo ambayo yeye anayahitaji kwenye Serikali yake.

Kadhalika Rais Magufuli alidai kuwa kuna watu hawafurahii maendeleo ya Tanzania, ndiyo maana wamekuwa wakijitahidi kufanya chokochoko.


“Nani afurahie nchi hii inayokaa kwa amani ninyi pale mmekaa, yupo wa ACT Wazalendo na wa CHADEMA yupo pale amekaa sawa sawa kila mtu na kila mahali wote, tunajiona ndugu kwa sababu maendeleo hayana chama,

Tunajenga hospitali ile huyu wa ACT atashindwa kwenda pale? barabara hii wa CHADEMA si ndiyo wanawahi kwenda kuandamana mle hayo ndiyo maendeleo ninayotaka ya nchi yangu, hayo ndiyo maendeleo ya Watanzania na ndiyo maana nawapongeza Wizara ya ujenzi kwa kumaliza ujenzi wa hii barabara”, alisema Rais Magufuli.

No comments: