Friday, October 23, 2015

TUNDURU KASKAZINI KUMCHAGUA MANJOLO



Na Steven Augustino,
Tunduru.

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Tunduru Kaskazini wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, wameanzisha utaratibu wa kupita nyumba kwa nyumba ili kumsaidia kufanya kampeni mgombea ubunge, kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Manjolo Kambili ambaye anaungwa mkono na UKAWA.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa masharti ya kutotajwa majina yao walisema, walisema kuwa maamuzi hayo wameyachukua baada ya kubaini kuwa mgombea ubunge aliyeteuliwa kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi, Mhandisi Ramo Makani  kuwa hawamtaki.

Walisema wamelazimika kuingia katika mapambano hayo, ili kuhakikisha kuwa mgombea huyo wa CCM, anang'olewa kupitia Sanduku la kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.


"Sisi ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi, hatuna mpango wa kuhama chama lakini hatumtaki Ramo", walisema.

Katika kampeni hizo walisema, wanawahamasisha wananchi wa Jimbo hilo kumchagua mgombea wa CUF katika nafasi ya ubunge, rais na diwani.

Walisema Ramo amekuwa akikigawa chama, katika makundi ya  walionacho na wasionacho kwa ajili ya manufaa yake binafsi, na kusababisha jimbo kupoteza viti vingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka 2014. 

Katika kipindi ha uongozi wake anadaiwa kuwa miaka mitano  aliyopewa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao mwaka 2010, aliahidi kutoa nafasi kwa mwanamke mmoja kila kijiji katika  jimbo hilo kwenda kusomea mafunzo ya ujasiriamali, na kutoa pikipiki kwa vijana waliomsaidia kampeni lakini hai leo hii ahadi hizo hajazitekeleza.

No comments: