Tuesday, October 6, 2015

WASHIKILIWA KWA KOSA LA KUJIANDIKISHA MARA MBILI KATIKA BVR

Revocatus Malimi, kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma. 
Na Muhidin Amri,
Ruvuma.

JESHI la Polisi mkoani Ruvuma, linawashikilia watu 18 kwa  kosa la kujiandikisha zaidi ya mara mbili katika daftari la kudumu la wapiga kura,  kwa njia ya kielektroniki (BVR).

Kukamatwa kwa watu hao, kumetokana na ushirikiano kati ya Jeshi hilo na taasisi nyingine zinazohusika na uandikishaji huo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Revocutus Malimi alisema kwamba watu hao wamekamatwa kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo, hata hivyo bado wanaendelea kuwatafuta wengine ambao wanadaiwa nao kujiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari hilo.


Malimi alieleza kuwa kati yao wapo watumishi wa idara ya serikali, wanafunzi, wakulima, wafanyabiashara na watu wa kawaida ambapo katika wilaya ya Songea wamekamatwa watu nane.

Wilaya ya Tunduru watatu, ambao tayari wamefikishwa Mahakamani, wilaya ya Mbinga watu watano na Nyasa wamekamatwa watu wawili ambao nao wamefikishwa Mahamani, kujibu mashitaka ya kosa hilo walilolifanya.


No comments: