Saturday, December 9, 2017

BABU SEYA PAPII KOCHA WATOKA GEREZANI JIONI HII

Mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) pamoja na mwanaye Papii Kocha wakipunga mikono baada ya kutoka katika Gereza kuu la Ukonga jijini Dar es salaam walikokuwa wanatumikia kifungo cha maisha na sasa wameachiwa huru kwa msamaha wa Rais Dokta John Pombe Magufuli alioutoa leo huko mjini Dodoma kulikofanyika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Babu Seya na mwanawe ni sehemu ya wafungwa 8,157 waliopata msamaha wa Rais.
Babu Seya akitoka gereza kuu la ukonga jioni hii ya leo.



Baadhi ya mashabiki wa wanamuzi wakiwa nje ya gereza la Ukonga Dar es Salaam wakimsubiri mwanamuziki Nguza Viking na mtoto wake Papii Kocha waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela na sasa wamepata msamaha. (Picha na Said Mwinshehe, Globu ya Jamii).


 

No comments: