Friday, December 8, 2017

MAGUFULI KUPAMBANA NA WATAKAOJIHUSISHA NA RUSHWA CHAGUZI ZA JUMUIYA DODOMA

Dodoma.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dokta John Pombe Magufuli, ametoa onyo kali kwa watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu wa Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ndani ya CCM.

Hayo alisema leo mjini Dodoma wakati akizindua mkutano wa tisa wa wa Umoja huo huku akieleza kuwa hatosita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kutumia mbinu za ujanja ujanja ikiwemo rushwa ili achaguliwe.

“Nikigundua kulikuwa na ukiukwaji katika uchaguzi huu nitachukua hatua na hili ni kwa UVCCM, UWT, Wazazi na jumuiya nyingine, kwa sababu mimi sikupita kwa rushwa kama kuna mchezo huo mchafu ulifanyika tutakaa na tutafuta huo uchaguzi”, alisema.

Alifafanua kuwa wamchague kiongozi kwa kumtanguliza Mungu ambaye ataweza kuwa mtetezi wa akina mama na atakayeweza kuthamini kanuni na katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Haiwezekani tukawa na viongozi ambao wametekwa na watu wengine kwa maslahi ya mambo fulani, niwaombe wanaCCM wenzangu tunafahamu UWT iliyokuwa ya akina Sophia Simba, siyo UWT tuliyo nayo sasa nawapenda akina mama naomba mnisaidie katika hili mtakayemchagua awe anajitambua kwamba kuongoza ni kuwatumikia anaowaongoza.

 

 

No comments: