Monday, December 18, 2017

ROSE MUHANDO AJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI



MUIMBAJI wa nyimbo za Injili, Rose Muhando leo amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mbele ya Mkutano Mkuu wa tisa wa chama hicho unaoendelea kufanyika mjini Dodoma.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole amethibitisha hayo wakati akimkaribisha Muimbaji huyo.

“Mheshimiwa Mwenyekiti wa muda, ndugu yetu Rose Muhando pamoja na kundi lake wamekuja na maombi mawili, 

“Moja ni kuimba wimbo maalum kwa ajili ya Rais lakini ombi la pili ni kujiunga na CCM, hivyo wataimba halafu watazungumza kisha nitawakabidhi kwa Makatibu kwa ajili ya utaratibu”, alisema Polepole.

No comments: