Wednesday, December 27, 2017

RAIS MAGUFULI ATUNUKIWA TUZO YA AMANI

Dokta John Magufuli.


JOHANNESBURG, Afrika Kusini.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa katika kijamii.

Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka 2017 ilipokea maombi ya wa wania tuzo 4,956.
Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.

Kadhalika Mahakama ya juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa ujasiri kwa masilahi ya mataifa yao.


Rais wa taasisi ya Mandela, Dokta Paul Kananura alisema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka husika.

Mahakama ya juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya Urais katika uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu yaliyompatia ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.

“Hii inaonesha kuwa Rais Kenyatta amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya”, alisema Dokta Kananura.

Rais wa Chad, Idriss Itno naye amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na ziwa Chad.

Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).

No comments: