Monday, December 18, 2017

TAKUKURU YAMUACHIA RAIS WA WALIMU



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) hapa nchini imemuachia aliyekuwa Rais wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) Gratius Mukoba bila kumfikisha Mahakamani.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga  alisema kuwa Mukoba hakupelekwa Mahakamani kama ilivyotakiwa.

“Hapana hatujampeleka Mahakamani, tulikwisha muachia ni hivyo kwamba Mahakamani hakupelekwa”, alisema Kuhanga.

 
Mwishoni mwa wiki taasisi hiyo ilimkamata Mukoba kwa madai ya kujihusisha na ugawaji wa rushwa kwa wajumbe na alitarajia kufikishwa Mahakamani leo.

Kadhalika alipoulizwa iwapo Rais huyo wa zamani wa CWT ataitwa tena au taasisi yake imeona hana hatia, Kamanda Kuhangwa alisema; “wewe elewa kuwa hatujampeleka Mahakamani lakini tumemwachia”.

No comments: