Sunday, December 24, 2017

MAJALIWA AWASHUKIA MADIWANI SONGEA ASISITIZA WASIPOMALIZA TOFAUTI ZAO ATAWAFUKUZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Na Kassian Nyandindi,     
Songea.

MADIWANI katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, wametakiwa kuachana na makundi yanayoigawa Manispaa hiyo kwani endapo wakiendelea kufanya hivyo wamekuwa wakikwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema hayo jana wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya siku moja katika mkoa huo.

Majaliwa alisema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi pamoja na Madiwani hao mjini hapa, ambapo aliwaambia endapo kama watashindwa kumaliza tofauti zao yeye atawafukuza.


“Madiwani mnaigawa halmashauri, pamoja na nguvu mliyonayo ya kuiendesha halmashauri lakini mnaiendesha vibaya, miradi haijengwi vizuri mmeingiza maslahi yenu binafsi wakati mwingine pesa zinatumwa mnaanza kubishana tu, sasa ni mwisho mkiendelea tutawafukuza, alisema Majaliwa.

Alibainisha kuwa Serikali inakusanya kodi ili wananchi waweze kupata maendeleo lakini wao wanachelewesha miradi ya maendeleo kwa malengo ya kuikwamisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo hatakubali na atawafukuza.

Hata hivyo alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Tina Sekambo kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtaka kuripoti kwake endapo pesa zitaingia kisha Madiwani kuanza kubishana bila utekelezaji ili awashughulikie hata kama atakuwa ni Meya wa Manispaa hiyo.

No comments: