Monday, December 18, 2017

MKAPA KUONGOZA UCHAGUZI MWENYEKITI MPYA CCM



Dodoma.

RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ameteuliwa muda huu mjini Dodoma kuwa Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuongoza uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Hatua hiyo inatokana na Rais John Magufuli kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho tawala, ili kupisha taratibu za uchaguzi wa nafasi hiyo.

Chama cha mapinduzi hufanya chaguzi zake, ikiwa ni pamoja na kumchagua mwenyekiti kila baada ya miaka mitano.

No comments: