Monday, December 4, 2017

HOJA PROJECT NA MIKAKATI YA KUKUZA ELIMU RUVUMA

Na Mwandishi wetu,  
Songea.

HOJA Project ni asasi ambayo isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake makuu mjini Songea, mkoani Ruvuma inatarajia kutumia kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali ya chuo cha ualimu mkoani humo.

Kadhalika ujenzi wa baadhi ya majengo ya chuo umeanza kujengwa ikiwa ni pamoja na majengo ya utawala, ukumbi, vyoo, mabweni ya kulala wanafunzi pamoja na mabanda kwa ajili ya kufugia mifugo.

Mratibu wa COCO Tanzania ambaye ni Meneja mkuu wa miradi ya katika sasi hiyo, Oswin Mahundi alisema hayo mjini hapa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake.

Alisema kuwa ujenzi wa majengo hayo utakapokamilika utaanza kutoa mafunzo mbalimbali kwa ngazi ya stashahada na cheti katika fani ya ualimu, usimamizi wa biashara, ukarani, kompyuta, kilimo, uhasibu, maendeleo ya jamii na masuala ya utalii.

Mahundi alieleza kuwa chuo hicho kinatarajia kuchukua wanafunzi kuanzia mwaka 2018 ambapo aliiomba Serikali kutoa ushirikiano na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa hiyo katika kujiendeleza.

Pia alifafanua kuwa Hoja inamiliki na kuendesha shule za sekondari mbalimbali ikiwemo shule ya Hoja sekondari na shule ya sekondari Mshangano zote zilizopo katika Manispaa ya Songea, shule ya sekondari Kindimba juu iliyopo wilaya ya Mbinga pamoja na kituo cha elimu kiitwacho Elimika.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakishirikiana na jamii na asasi zingine za kijamii kuendesha shule za chekechea ambazo ni Olamayani nursary school iliyopo Monduli mkoani Arusha, MCODE mkoani Kilimanjaro, MLASEO mkoani Pwani, Lupembe mkoani Njombe, Kids are kings iliyopo Manispaa ya Songea na Litisha Songea vijijini.

Pamoja na mambo mengine, Hoja project ilianza kama wazo mnamo mwaka 2005 chini ya mratibu huyo kwa kupitia magumu katika safari yake ya elimu kwa nia ya kujenga shule ambazo itasaidia kusoma bure watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha au kwa gharama nafuu.

No comments: