Friday, December 8, 2017

WAZIRI JAFO AMTUMBUA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUISABABISHIA HASARA SERIKALI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Seleman Jafo akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Dodoma juu ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Nkasi, Julius Kaondo.
Na Mwandishi wetu,
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Seleman Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji Wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa, Julius Kaondo kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya shilingi bilioni 7.

Hatua hiyo ya Waziri Jafo kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo alisema kuwa imefuatia baada ya kushindwa kusimamia alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.

Taarifa za kusimamishwa huko zilielezwa leo na Waziri huyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Dodoma mjini hapa.


“Natumia sheria ya Serikali za Mitaa sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka haya”, alisema Jafo.

Jafo aliongeza kuwa fedha hizo zilikuwa za mradi wa maji wa kijiji cha Kamwanda wilayani humo, ambako Mkurugenzi Kaondo anadaiwa kushirikiana na mmoja wa maofisa kutoka Wizara ya maji kuhujumu fedha za mradi huo.

Hata hivyo amemuomba Waziri wa Maji na umwagiliaji, Issack Kamwelwe kumchunguza mmoja wa watumishi katika Wizara yake ambaye analalamikiwa kushirikiana na Mkurugenzi huyo kuhujumu mradi huo.


 

No comments: