Thursday, December 21, 2017

VYAMA TISA KUPAMBANA UCHAGUZI NAFASI YA UBUNGE SONGEA



Na Muhidin Amri,      
Songea.

VYAMA tisa vimejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mdogo wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma.

Tina Sekambo.
Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Tina Sekambo amevitaja vyama ambavyo hadi sasa tayari vimekwisha jitokeza kuchukua fomu hizo kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), UPDP, Demokrasia Makini, AFP, TLP, CCK, NRA, ADA na TADEA.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hadi kufikia jana bado hakikujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi huo, ambao unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Leonidas Gama wa CCM kufariki dunia mapema mwezi uliopita.


Pia Sekambo alieleza kuwa mwisho wa kuchukua  na kurudisha fomu hizo ilikuwa ni Desemba 20 mwaka huu majira ya saa 10  huku akisisitiza kuwa Ofisi yake haitakuwa tayari kutoa na kurudisha fomu baada ya muda huo.

No comments: