Monday, January 29, 2018

JAJI MKUU AZINDUA KITUO CHA MAFUNZO NA HABARI ZA MAHAKAMA



Na Mwandishi wetu,
Dar es Salaam. 

JAJI Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amezindua kituo cha mafunzo na habari za Mahakama ili kuwajengea uwezo watumishi.
Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma.

Akizindua kituo hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Januari 29 mwaka huu, Profesa Juma alisema malengo ya kufanya hivyo ni kuhakikisha haki inawafikia wananchi kwa wakati na kwa urahisi zaidi.

Profesa Juma alisema kituo hicho kimejengwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia.

Jaji Mkuu alifafanua kuwa wanawajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwa sababu kuna mambo mengine hawakusoma wakiwa chuoni.


Alisema kuwa Tehama inarahisisha kazi kwa kutoa haki kwa wakati na kwa urahisi, pia kuwafikia wananchi.

Maeneo mapya yanayotakiwa kufanyiwa kazi na watumishi wa Mahakama alieleza kuwa ni makosa ya mtandao, yanayotokana na miamala ya simu na dawa za kulevya.

Jaji Mkuu, Profesa Juma alisema Mahakimu na waendesha mashtaka wakipata mafunzo watakuwa na uelewa mmoja katika kutoa haki.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird akizungumzia mfumo huo wa Tehama alisema utasaidia kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi na watapata haki kwa wakati.

No comments: