Wednesday, January 24, 2018

MWALIMU MBARONI KWA TUHUMA YA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MLEMAVU



Na Mwandishi wetu,
Kilwa.

MWALIMU mmoja wa shule ya wanafunzi wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, amefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafunzi mwenye ulemavu na kumsababishia ujauzito.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai.

Akizungumza katika kongamano la Wadau wa elimu lililoandaliwa na shirika la TCRS, Mkuu wa Wilaya Kilwa, Christopher Ngubiagai alisema kuwa kitendo hicho kilichofanywa na mwalimu huyo sio cha kukifumbia macho huku mwanafunzi aliyefanyiwa hivyo akiwa amekatisha kuendelea na masomo yake.

Ngubiagai alieleza kuwa Wilaya hiyo imekuwa akiathirika na tatizo la mimba za utotoni na utoro kwa wanafunzi mashuleni na husababisha watoto hao kufanya vibaya katika mitihani ya Kimkoa na Kitaifa.


Wilaya ya Kilwa imeshika nafasi ya sita kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Lindi katika matokeo ya mitihani darasa la saba mwaka jana, huku ikishika nafasi ya 160 Kitaifa.

No comments: