Wednesday, January 31, 2018

SERIKALI YATOA GHARAMA MPYA HATI YA KUSAFIRIA



WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi, Dokta Mwigulu Nchemba amesema kwamba gharama mpya ya hati ya kusafiria ya Kielektroniki itakuwa ni shilingi 150,000.

Hayo yalisemwa leo na Dokta Nchemba wakati wa uzinduzi wa hati hiyo jijini Dar es Salaam, ambapo imezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli.

Vilevile Dokta Nchemba alisema kuwa hati hizo za kusafiria (Pasipoti) zitakuwa na ukurasa zaidi ya mmoja na mwonekano mpya.


Hata hivyo Rais Magufuli alisema kuwa gharama ya laki moja na nusu bei hiyo ni ya juu kidogo kuliko bei ya sasa, huku akieleza kuwa bei hiyo imezingatia ubora wa utengenezaji wa Pasipoti hiyo.

No comments: