Monday, January 1, 2018

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA BABA WA ASKOFU NZIGILWA



MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza kuaga mwili wa Alfred Nzigilwa, ambaye ni baba mzazi wa Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa katika ibada iliyofanyika Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea.

Mzee Nzigilwa (87) alifariki dunia Desemba 29,2017 nyumbani kwake Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa alikuwa akipata matibabu mara kwa mara katika hospitali za Muhimbili, Madonna na Regency kutokana na maradhi ya tumbo na moyo kutanuka.


Viongozi kadhaa wamemuelezea mzee Nzigilwa wakisema alikuwa mmoja wa viongozi mahiri wa kanisa kwa muda mrefu na alikuwa msaada katika usuluhishi wa migogoro ya ndoa.

Padri Stephano Kaombe amesema msiba huo umekuwa na sura ya kijimbo kwa sababu ya nafasi ya Askofu Nzigilwa lakini pia kwa maisha aliyoishi mzee huyo.

Mazishi yamefanyika leo Jumatatu Januari Mosi, 2018 katika makaburi yaliyopo Pugu jijini Dar es Salaam.

Mwananchi.

No comments: