Wednesday, January 31, 2018

RAIS MAGUFULI AWATAKA UHAMIAJI KUENDELEA KUSHUGHULIKIA WAHAMIAJI HARAMU



Na Mwandishi wetu,

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli ameitaka idara ya Uhamiaji hapa nchini kuendelea kushughulikia wahamiaji haramu pasipo kumwogopa mtu yeyote yule.

Dokta Magufuli alitoa agizo hilo leo wakati alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa hati ya kusafiria ya Kielektroniki jijini Dar es Salaam, huku akiipongeza Wizara ya mambo ya ndani kwa utendaji mzuri wa kazi.

Alisema kuwa Wizara hiyo anaipongeza kwa sababu Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo wakati anamteua alimpeleka pale akimwambia kwamba kuna changamoto nyingi na kwa kiasi kikubwa sasa zimetatuliwa.


“Na ndio maana Kamishna wa imagration alivyoniambia kuwa wanahitaji nyumba  za wafanyakazi kule Dodoma sijatoa kwa taasisi nyingine nyumba, lakini nilitoa hela Serikalini tukatoa nyumba 103  kule Dodoma  ni kwasababu ya uzalendo ambao nimeanza kuuona,

“Lakini pia mimi nimejiandaa kuja kutoa hela nyingine makao makuu mmeshakubali kuhamia Dodoma na hapa palivyokaa kaa hapa hapakai kama makao makuu ya imagration, ninajua kuna baadhi ya wafanyakazi watalaumu kuhamia Dodoma”, alisema.

Alisema kuwa atawapatia bilioni 10 wakati wowote kuanzia sasa ili waweze kuanza kazi ya ujenzi wa Ofisi za makao makuu ya Uhamiaji Dodoma.

“Ni lazima tuwe na jingo zuri  katafuteni eneo  nitawapa bilioni 10 wakati wowote mtakapozihitaji muanze kujenga makao makuu na ninatoa hivi kwa shukurani mnayofanya kwa utendaji wenu mzuri wa kazi endeleeni kuchapa kazi na kushughulikia wahamiaji haramu bila kumuogopa mtu yeyote”, alisema Dokta Magufuli.

No comments: