Tuesday, January 16, 2018

YANGA YALAMBA DILI LA BILIONI MBILI



MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Yanga, leo wamesaini mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo, Macron wenye thamani ya shilingi bilioni mbili.

Katika mkataba huo uliosainiwa kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Yanga itatoa haki zote za utengenezaji na usambazaji wa jezi zao huku pia nembo ya kampuni ya Macron, itaanza kuonekana kwenye jezi za Yanga SC.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amewaonya wote wanaouza jezi za klabu hiyo bila kuwepo kwa makubaliano watawachukulia hatua za kisheria kwa sababu sasa yupo mwenye haki ya kufanya hivyo. 


Pia Mkwasa amewakaribisha wawekezaji zaidi ndani ya klabu hiyo.

Naye Mkurugenezi Mtendaji wa kampuni hiyo hapa Tanzania, Suleiman Karim amewahakikishia wanayanga kuwa klabu hiyo itapata faida kupitia mauzo ya jezi orijino za klabu.

Kampuni ya Macron inafanya kazi katika nchi zaidi ya 16 duniani ikiwemo England, Italia na Ufaransa. 

Hivi karibuni kampuni hiyo iliingia mkatata wa miaka 2 na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wenye thamani ya shilingi milion 800.

No comments: