Wednesday, November 14, 2012

MPAKA WA UGANDA NA DRC KUFUNGWA

Waasi wa M23














Serikali ya Uganda imetangaza kufunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kivuko cha Bunagana.

Hatua hiyo ya serikali ya Uganda inajiri baada ya ripoti moja ya Umoja wa Mataifa kuishutumu Uganda kwa kuwaunga mkono waasi wa M-23 wanaopigana na serikali katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Uganda na Rwanda zimepuuza kabisa ripoti hiyo.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Kanali Felix Kulaigye, amethibitisha amri ya kufungwa kwa mpaka huo iliyotolewa na rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Eneo hilo la mpakani la Bunagana ni muhimu kwa usafirishaji bidhaa zinazotumiwa na wapiganaji wa kundi hilo la waasi wa M-23.(BBC News)

No comments: