Monday, November 12, 2012

WASIWASI WATANDA BAADA YA MAUAJI KENYA

Ramani ya kenya.



















Wanavijiji nchini Kenya kaskazini wanahofia kuzuka kwa mapigano zaidi baada ya takriban polisi 29 kuuwawa mwishoni mwa wiki.

Polisi hao walivamiwa walipokuwa wanajaribu kurudisha ng'ombe waliokuwa wameibwa.
"Tunahofia kwamba maafisa wa ulinzi waliojawa na hasira huenda wakawashambulia wananchi wasio na hatia kwani waliowaua polisi hao wameshatoroka," alidokeza kiongozi huyo.

Aidha alisema kwamba kungali kuna miili mingine ambayo haijapatikana.

Wasamburu na Waturkana huibiana mifugo mara kwa mara. Pia hupigania maeneo ya lishe kwa mifugo na maji.

Kulingana na waandishi habari wa Kenya, majuma mawili yaliyopita watu 12 waliuwawa katika tukio kama hilo karibu na mahala hapo.(BBC News)

No comments: