Monday, November 12, 2012

WANAJESHI ZAIDI YA 3,000 KUTUMWA MALI




Mawaziri wa ulinzi wa Afrika Maghahibi wakijadiliana mkakati wa kijeshi nchini Mali.







Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi wamekubali kupeleka kikosi cha wanajeshi 3,300 nchini Mali kuweza kutwa udhibiti wa eneo la Kaskazini kutoka kwa wapiganaji wa kiislamu.

Kwenye mkutano wa nchi wanachama wa shirika la Ecowas, mwenyekiti wa shirika hilo, alisema liko tayari kutumia nguvu kupambana na makundi ya kigaidi pamoja na mitandao ya uhalifu.
Wanajeshi watatolewa na Nigeria, Niger na Burkina Faso.
Makundi ya kiislamu na waasi wa Tuareg walichukua udhibiti wa eneo la Kaskazini mwa Mali baada ya aliyekuwa Rais Kupinduliwa mwezi Machi.

Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara aliambia waandishi wa habari nchini Nigeria kuwa wanajeshi wataanza kazi pindi Umoja wa Mataifa utakapoidhinisha mkakati huo wa kijeshi.

Aliongeza kuwa anatumai baraza la usalama litaidhinisha mpango huo mwishoni mwa Novemba na Disemba.

Kulingana duru za jeshi la Mali, mpango huo utachukua kipindi cha miezi sita huku kukiwa na maandalizi mwanzo kabla ya mafunzo kwa wanajeshi hao, pamoja na kuandaa kambi zao na kisha baadaye jeshi kuanza harakati zake Kaskazini mwa nchi.

Umoja huo ulikuwa umetoa muda wa siku arobaini na tano kwa viongozi wa Afrika kuanzia tarehe 12 mwezi Oktoba kuunda mkakati wa kijeshi kuweza kuingilia kati mzozo unaoendelea Kaskazini mwa nchi.(BBC News)

No comments: