Monday, November 5, 2012

JENGO HILI LIFANYIWE UKARABATI ILI WANAFUNZI WAWEZE KUWA NA MAZINGIRA MAZURI YA KUSOMEA


Hili ni moja kati ya jengo chakavu la shule ya msingi Masumuni iliyopo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, ambalo halina madirisha na sakafu yake ni ya vumbi ambapo walimu na wanafunzi wamelalamikia halmashauri ya wilaya hiyo kutolifanyia ukarabati kwa zaidi ya miaka sita huku wanafunzi wakiendelea kulitumia wakati wa  masomo. (Picha na Kassian Nyandindi).



KWA UFUPI:

Shule ya Msingi Masumuni ni shule ambayo ipo kata ya Mbinga mjini, nimeshuhudia shule hiyo wanafunzi wanavyotaabika kutokana na tatizo la vyoo na upungufu hata wa madawati ya kukalia wakati wanapokuwa darasani masomoni, ni vyema sasa uongozi husika ukalifanyia kazi suala hili ili kunusuru hali hiyo isiweze kuendelea. 

No comments: