Tuesday, November 27, 2012

TAARIFA YA KIFO CHA SHARO MILIONEA HII HAPA

Sharo Milionea afariki dunia mkoani Tanga.

















Msanii na mwigizaji maarufu nchini Tanzania Sharo Milionea amefariki dunia leo saa 2:00 usiku mkoani Tanga kwa ajali ya gari.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga, amesema kwamba msanii hiyo amepata ajali saa 2:00 usiku tarehe 26, Novemba, 2012.

“Leo majira ya saa 2:00 usiku kwenye Barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza,


"alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza, gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”, amesema Kamanda huyo.


Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea ambako ni  katikati ya Segera na Muheza.

Mtandao wa www.habarimasai. com umeelezwa kwamba gari limehifadhiwa mahali salama na halitembei. Katika gari hiyo alikuwa mwenyewe. (Source Habari Masai)

No comments: