Saturday, November 10, 2012

HATARI! VIONGOZI MPO WAPI JUU YA TATIZO HILI ?

Hivi ni vyoo ambavyo vinatumiwa na wateja wanaokunywa pombe za kienyeji katika kilabu cha Manzeshe, kilichopo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma. Vyoo hivi vimefurika kinyesi (Vimejaa) na kuhatarisha usalama wa afya za watumiaji huku uongozi husika wa halmashauri hiyo ukiona tatizo hilo na kutochukua hatua za haraka kunusuru hali hiyo. wateja wamekuwa wakiendelea kuvitumia licha ya vyoo hivyo kuwa katika hali mbaya.(Picha na Kassian Nyandindi)

No comments: