Wednesday, November 28, 2012

WAKAMATWA KWA PESA HARAMU

WAZIRI wa mambo ya ndani wa Bolivia, Carlos Romero amesema, kuwa maafisa kadhaa wa serikali wametiwa mbaroni kwa kujaribu kupokea pesa kutoka kwa mfanyibiashara mmoja kutoka Marekani ambaye anahudumia kifungo cha jela nchini humo.

Wale waliokamatwa ni pamoja na Mkurugenzi wa maswala ya kisheria katika wizara ya mambo ya ndani Fernando Rivera.


Mfanyibiashara huyo wa mjini New York , Jacob Ostreicher, alikamatwa mwaka uliopita kwa kosa la kuhamisha pesa nyingi bila kibali baada ya kuekeza dola milioni ishirini na tano katika biashara ya uzalishaji wa mpunga nchini Bolivia.

Amesema mashtaka dhidi yake ni hila ya kutaka kumpokonya pesa zake.(BBC News)

No comments: